Archive for November, 2005
Bendera ya Uingereza yafanyani katika tovuti ya CHADEMA?
November 23, 2005UKIMWI bado ni tishio
November 22, 2005Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia UKIMWI, UNAIDS kwa kushirikiana na Shirika la Afya duniani, WHO limetoa taarifa ya mwaka inayoonyesha jinsi UKIMWI ulivyo bado ni tishio hasa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Unaweza kuisoma taarifa hiyo kwa kubonyeza hapa
Kiswahili kitolewe utumwani kwanza
November 18, 2005Jeff Msangi kaanzisha mjadala wa kiswahili katika blogu yake. Ametoa hoja za msingi ambazo zaweza kujadiliwa. Ili mjadala ule unoge naongezea makala iliyoandikwa na Prudence Karugendo anayetoa hoja kwamba tuanze kukitoa kiswahili utumwani kwanza. Hoja yake ni kwamba kiswahili kimeazima maneno mengi sana ya kiarabu wakati tuna lugha kwa mamia za kibantu ambazo tungeweza kutumia maneno yake na kubadilisha mengi ya kiarabu. Soma makala yake hapa na mjadala uendelee.
Uvutaji na unywaji wa pombe na Saratani tena
November 18, 2005Saratani yazidi kuongezeka shauri ya kubwia pombe
November 16, 2005Soma habari hii inayotoa onyo juu ya ongezeko la saratani kutokana na kunywa kupindukia. Bonyeza hapa
Uhuru si urithi
November 15, 2005Nimekutana na nukuu hii:
“No people are really free until they become the instrument of their own liberation. Freedom is not a legacy that is bequeathed from one generation to another. Each generation must take and maintain its freedom with its own hands.” By John Henrik Clarke
Kila kizazi inabidi kipambane kujipatia uhuru wake.
Makala za Prudence
November 13, 2005Mzalendo mmoja aitwaye Prudence Karugendo amenitumia makala zake ambazo angependa zisomwe na watanzania wengine ili kubadilishana mawazo na kuleta changamoto katika kujadili mustakabali wa nchi yetu. Nimeweka kona ya makala zake kwenye blogu hii chini ya Kona ya Padre Karugendo. Hawa ni watu wawili tofauti. Mmoja ni Privatus mwingine ni Prudence. Kwa leo naweka makala zake tatu. Moja inaitwa kiini macho cha kusamehewa madeni. Pamoja na mambo mengine anaongelea misamiati migumu inayotumiwa katika kuandika mambo ya kiuchumi. Anahoji pia kwa nini tunaambiwa sasa tusherehekee kusamehewa madeni wakati ambao hatukuambiwa yalikopwa lini, na nani, kwa ruhusa ya nani na yalifanyia nini? Isome hapa. Nyingine mbili zinahusu amani. Moja anauliza kama kweli Tanzania kuna amani au ni kiini macho cha amani. Isome kwa kubofya hapa. Nyingine anauliza je ni upinzania au chama twawala kinachohatarisha amani? Isome hapa
Tanzania yaingizwa kwenye kapu la Misaada mingine ya Marekani
November 11, 2005Tanzania imefanikiwa kuingizwa katika mpango wa misaada wa Marekani unaoitwa Millenium Challenge Corporation (MCC). Ili uingizwe humo ni lazima kwanza uwe na utawala bora kwa vigezo vya jamaa wa Benki ya Dunia na Wizara ya Fedha ya Dunia (International Ministry of Finance), wenyewe wanaita International Monetary Fund. Sasa tungoje majivuno na matusi toka kwa mwenyewe. “Wale wote mnaosema nchi haina utawala bora ni vipofu. Hamuoni hata Marekani inatambua? Nyie watanzania msioona ni watu wa ajabu sana”. Tutayasikia haya karibuni. Soma Hapa habari hiyo.
Wanywaji wa Kahawa Huree
November 9, 2005Tafiti zinachanganya Kweli. Tofauti na inavyoaminika kwamba kunywa kahawa kwa wingi husababisha Magonjwa ya moyo, utafiti mpya umegundua kwamba unywaji wa Coca Cola unaweza kuwa hatari zaidi. Soma hapa
Makala kuhusu Askari kuwachapa Raia
November 9, 2005Bwana Sakito Mallya ameandika maoni yake kuhusu Askari wa Tanzania kuwapa kipigo raia. Makala hiyo ilitoka kwenye Gazeti la Rai la tarehe 3/11/2005. Unaweza kuisoma kwa kubonyeza hapa