Njaa ya Bara la Afrika ni ya kujitakia?

BBC iliendesha mdahalo mzuri sana kati ya Nicholas Crawford toka WFP na Tajudeen Abdul-Rahem Wa Justice Afrika kuhusu chakula barani Afrika. Jamaa wa Justice Afrika anadai kwamba hakuna haja ya Afrika kupewa msaada wa chakula na anajaribu kuelezea kiini cha tatizo la njaa barani Afrika na jinsi misaada inavyolemaza bara hili. Mzungu wa WFP anatetea umuhimu wa msaada wa chakula. Kwa kweli nakusihi usome mdahalo huo hapa. Ni mdahalo poa mno

3 Responses to “Njaa ya Bara la Afrika ni ya kujitakia?”

  1. Ramadhani Msangi Says:

    Ukengeufu wa kimawazo na kiakili ni umasikini mkubwa sana humu duniani kinyume na watu wanavyodhania na kuacha kujadili upande huu. Suala la kuwa miradi inadumaza waafrika au kuwaendeleza ni suala la mapokeo zaidi kuliko ukweli wenyewe. Kwakusema ukweli ni kuwa Afrika tuna kila kitu kwa ajili ya kutufanya tusife njaa, ikiwa ni pamoja na mabonde yenye rutuba na mito ya kutosha, lakini tunahitaji kujenge miundombinu kwa ajili ya kuwezesha hili, na ujenzi huo unahitaji fedha ambazo zinaweza kupatikana kupitia hao jamaa.

    Suala la kujadili ni kuwa je, kuna uwiano baina ya ukubwa wa miradi husika na fedha ambazo wanatoa hao jamaa, ambazo nyingi zinaelekezwa katika kufanya semina za elezo sijui na vu=itu kama hivyo?

  2. popolicious Says:

    i cant understand what the f*ck it says on your blog….

  3. Ferinannnd Says:

    Навеяно наверное стандартным мышлением? Будьте проще ))

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Connecting to %s


Follow

Get every new post delivered to your Inbox.