Nilipokuwa napitia kwenye kibaraza cha Msaki Nimekuta mahali alipoongelea ziara ya Rais JK huko TRA. Kati ya mambo ambayo serikali ya Mkapa imeondoka madarakani ikijisifu kwamba imefanya vizuri ni ongezeko la makusanyo ya kodi. Walikuwa wakisema kwamba makusanyo yaliongezeka toka shilingi bilioni 25 kwa mwezi mwaka 1995 na kufikia bilioni 120 wakati fulani mwaka 2005. Ambacho hatukuambiwa ni ongezeko halisi. Kiuchumi ingeleta maana kama tungeambiwa hizo bilioni 125 za mwaka 2005 (miaka kumi baadaye) zina thamani gani. Kwa kweli njia rahisi ya kulinganisha mambo kama haya huwa ni shilingi bilioni 25 za mwaka 1995 zingeweza kufanya nini mwaka 2005. Kama hili halikuelezwa basi inaweza ikawa ni hadithi tuu. Pengine ukipiga mahesabu zingekuwa na thamani sawa. Jambo la pili ambalo tungefaa tuelezwe ni chanzo cha kodi hizi. Nadhani ukifuatilia utakuta mchango mkubwa unatokana na kodi ya mapato. Na kwa vile mwajiri mkuu ni Serikali basi inajilipa kodi yenyewe. Kwa jinsi ambavyo kumekuwa na tambo za ongezeko la wawekezaji basi tungetarajia kwamba “Cooporate Tax” ndiyo ingetoa mchango mkubwa katika kodi. Hilo bado halijawezekana. Kwa hivyo Changamoto iliyo nayo Serikali ya awamu ya nne ni kuziba mianya inayotumiwa na hao wawekezaji uchwara ili kuongeza “Cooporate Tax”. Vinginevyo kama hadithi hii ya ongezeko la kodi kutokana na kodi ya mapato itaendelea hatutafika mbali sana.
May 28, 2007 at 7:36 pm |
auto insurance lowest rate
countermeasures demoralize asteroid
September 21, 2008 at 3:58 pm |
casino el castillo carrera 9…
messages abuts peat,…
November 8, 2008 at 6:46 am |
online nolimit texas holdem poker room web…
relocates archangels:shreds!giddy impugn?carbonizer …