Gregory yuko wapi?

Nilikutana na binti mmoja ambaye tulikuwa wote Jeshi la Kujenga Taifa (Ndesanjo huliita la kubomoa taifa) akaniuliza: Hivi Gregory yuko wapi siku hizi? Nikamuuliza Gregory gani? Akanishangaa akasema kumbe urafiki wenu uliishia jeshini? Nikamuuliza jina lake la pili ni nani? Akaniambia Macha. Ohh!! Nikamwambia nimemkumbuka sasa. Nikamwambia kwamba Macha alirudisha jina lake la Gregory kwa Mchungaji wake kama mmoja wa wahusika katika kitabu cha Pambazuko Gizani alivyotaka kurudisha jina lake la Paulo kwa Padre. Binti wa watu hoi. Nakumbuka Macha alipokuwa kwenye jitihada za kurudisha jina lake alikuwa akinishambulia kila siku nirudishe la kwangu pia ikiwa ni ishara ya ukombozi mpya. Kabla ya kurudisha jina lake Ndesanjo alikuwa akiitwa Gregory!!!

3 Responses to “Gregory yuko wapi?”

  1. ndesanjo Says:

    Nkya, umenikumbusha mbali kweli. Jina hilo itabidi siku niliandikie kitabu kabisa maana jina tu linaweza kuelezea historia nzima ya Waafrika na mahusiano na wageni toka Ulaya na Uarabuni.

  2. pambazuko Says:

    Ni lazima historia ya majina hayo yaandikwe. Unajua haya mambo yanachekesha wakati mwingine lakini yanahuzunisha sana. Mzazi anamwita mwanaye jina ambalo hata yeye mwenyewe hawezi kulitamka!!

  3. mloyi Says:

    Jina kalirudisha lakini wengi hawatakubaliana na haki yake ya kurudisha jina kwa mwenye nalo na yeye kuchukua na la kwake! bado wataendelea kumuita gregory.
    Wiki iliyopita nilimwandikia ndesanjo kumuomba ushauri, nina rafiki mmoja ni mmarekani mwafrika, yeye anaitwa ryan daley anataka kurudisha jina kwa mwenyewe na kuchukua jina lake, lakini hayajui majina ya kwao, Sikumbuki vizuri matakwa yake, maana ya jina alilotaka, lakini nilinukuu sehemu ya barua yake kwa ndesanjo, naomba uhamishie ile barua hapa, ili watu wengi zaidi wapate nafasi ya kutoa ushauri kuhusu lile jambo.
    Tujivunie majina yetu.
    Mloyi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Connecting to %s


Follow

Get every new post delivered to your Inbox.