Archive for January, 2006
Tumepoteza maelfu ya miaka ya elimu
January 19, 2006Vyama Viendeshwe na wanachama
January 19, 2006Ukweli ni kwamba kwanza kabisa chama ni kikundi cha watu wenye mwelekeo unaofanana au wanakubaliana kiitikadi. Kama ni kikundi basi inabidi kiendeshwe na hao wanachama. Hakuna haja ya kila mtanzania kuendelea kuendesha vyama ambavyo ni vya watanzania wachache sana. Hivi ni asilimia ngapi ya watanzania ni wanachama wa vyama vya siasa? Hili tulivalie njuga ili hii ruzuku ifutwe. Sioni kama eti ruzuku inasaidia kukuza vyama na hatimaye demokrasia. Kwanza hili suala la kufikiria demokrasia ni vyama vingi sijuhi limetoka wapi. Hata kama pesa hizi kinadharia zina lengo la kuimarisha vyama basi kinachoimarika ni kimoja tuu. Hata kama vingeimarika vyote, viimarishwe na wanachama wenyewe. Wanaopenda vyama wavichangie.
Hivi vyama vya upinzani ingebidi vianze kuchimba masuala ya msingi ambayo yanafanya CCM kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha. Kwa mfano mali ambazo CCM ilirithi wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanza. Angalia viwanja vya mpira kibao bado ni vya CCM, majengo mengi ambayo yalijengwa kwa kodi za wananchi bado ni ya CCM. Kwa nini mali hizo ziendelee kubaki za CCM? Tume ya Nyalali ilipendekeza kwamba mali hizo zirudishwe Serikalini lakini mpaka leo hakuna kilichorudishwa. Halafu jamaa wa upinzani wanakaa kukimbilia ruzuku ambayo kila mwaka itaendelea kuongezeka kw CCM huku ikipungua kwao, huku Chama hiki twawala kikiendelea kufaidika na mapato ambayo ni mali ya kila mtanzania. Pamoja na mambo mengine ya katiba na tume huru ya uchaguzi mimi nimeongele mambo mawili yanayohusu pesa.
Hili la ruzuku wanablogu wote tulivalie njuga. Vyama viendeshwe na wanachama hizo hela za ruzuku zikabiliane na kipindupindu au shughuli nyingine za kimaendeleo.